News & Events

Programu ya Kuendeleza Kilimo ya AFDP itachangia uhakika na usalama wa Chakula na Ajira - Dkt. Batilda

Mkuu wa Mkoa waTabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema, Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) itasaidia  katika upatikanaji wa mbegu za mazao zinazoweza  kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi na hivyo  kusaidia  uhakika na usalama wa chakula nchini.

Aidha Balozi Dkt. Batilda alisema Program hiyo ya AFDP itachangia pia upatikanaji wa ajira kwa watu wengi hasa vijana katika maeneo inapotekelezwa pamoja na kuinua pato la wananchi na Taifa kwa ujumla

Mheshimiwa Balozi Dkt. Batilda alisema hayo Mei 11, 2023 alipokutana na ujumbe kutoka IFAD walipokuwa katika ziara ya usimamizi na ukaguzi wa utekelezaji wa Programu hiyo ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) Mkoani Tabora 

Akielezea kuhusu utajiri katika shughuli za sekta za kilimo na ufugaji mkoani mwake, Balozi Dkt. Batilda alisema kuwa mkoa wa Tabora ni maarufu  na umenufaika kwa kilimo cha zao la Tumbaku na Ufugaji wa Nyuki ambao uzalisha asali inayyotumika na kuuzwa kwa wingi ndani na nje ya nchi.

Naye mtaalamu wa Tathmini na Ufuatiliaji katika Programu hiyo Bw. Bernard Ulaya aliopoelezea utekelezaji wa Programu hiyo mkoani Tabora, alisema programu  inaendeleza kituo cha kuzalisha vifaranga vya samaki kilichopo Mwamapuli wilayani Igunga, shamba la kuzalisha mbegu za mazao ya kilimo la Wakala wa Mbegu (ASA) lililoko Kilimi katika wilaya ya Nzega, na wilaya ya Uyui  na kwamba itapewa pia nafasi ya kuendeleza minyororo ya thamani kwa mazao ya Alizeti, Mahindi na Maharage.

  • Google+
  • E-mail
  • PrintFriendly