News & Events

Wilaya ya Igunga kunufaika na Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi

Halmashauri ya Wilaya ya Igunga iliyopo mkoani Tabora imetajwa kuwa miongoni mwa wilaya kadhaa nchini zitakazonufaika na Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayofadhiliwa na Mfuko wa Kimataifa wa kuendeleza Kilimo (IFAD).

Mratibu wa Programu hiyo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera Bunge na Uratibu, Bw. Salim Mwinjaka alisema hayo Mei 13, 2023 alipokutana na kuzungumza na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, wataalam pamoja na ujumbe kutoka AFDP ulipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea maeneo yatakayoteleza Programu hiyo.

Mratibu Mwinjaka alifafanua akisema: “wilaya ya Igunga mkoani Tabora itakuwa miongoni mwa wilaya zitakazopata fedha za utekelezaji wa Programu ya AFPD ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi, kupitia wizara ya Kilimo katika mwaka wa fedha wa 2023/ 24, ambapo kwa mwaka wa fedha unaofuata na kwa kuzingatia maandalizi ya Mpango wa Mapato na Matumizi ya bajeti kuwekwa vizuri zaidi, fedha hizo zitapelekwa moja kwa moja katika kila wilaya husika"

Katika ziara na mkutano huo, Mwenyekiti wa ushirika wa umoja wa wafugaji wa samaki Igunga (UWASAI) uliopo katika kata ya Mwamapuli Bw. Francis Mgaragu, aliishukuru Serikali kupitia wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu -Sera Bunge na Uratibu kwa kuwaletea mradi huo akisema "Mradi tumeupokea kwa mikono miwili, tunaahidi kutoa ushirikiano katika kuutekeleza mradi  ili kufikia malengo yaliyokusudiwa".

  • Google+
  • E-mail
  • PrintFriendly