DC Kasesela Afungua Warsha ya Kujenga Uelewa Kuhusu ASDP2
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela amefungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028.
Alisema kuwa ili kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo nchini wataalamu wote nchini wanapaswa kubadilishana ujuzi na kushauriana namna ya kuwa na kilimo chenya tija kuliko kuficha ujuzi walionao kwa muktadha wa maeneo husika pekee waliyopo hivyo ni vyema kutumia ujuzi wao kwa makubaliano na maelekezano kwani jambo hilo litachochea zaidi ukuzaji wa sekta ya kilimo nchini Tanzania.
Dc Kasesela ameyasema hayo wakati Akizungumza kwenye ufunguzi wa warsha hiyo inayofanyika katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa, warsha inayowahusisha Makatibu Tawala wasaidizi upande wa uchumi kutoka mkoa wa Iringa na Pwani na Maafisa kilimo wa mikoa, Meya wa Manispaa/Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa halmashauri za Manispaa/wilaya, Wachumi wa Manispaa/Wilaya na Maafisa Kilimo wa Manispaa/Wilaya kutoka Katika Halmashauri za Manispaa na Wilaya kutoka Mkoa wa Pwani na Dar es salaam.
Dc Kasesela ameeleza kuwa Programu hii ya ASDP 2 imeandaliwa baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ASDP 1 iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2006/2007 hadi 2013/201 huku akiwapongeza waandaaji wa warsha hiyo ambao ni OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kutaraji kutekelezwa na wadau mbalimbali kama vile Wizara za sekta ya kilimo, Wahisani, Sekta binafsi, Taasisi zisizo za kiserikali, Wakulima Wafugaji, na Wavuvi.
Dc Kasesela amesema kuwa Utekelezaji wa ASDP 2 utazingatia malengo ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016-2021), Mkakati wa Taifa wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Dira ya maendeleo ya Tanzania (2025).
Alisema kuwa Programu hiyo imezingatia vipaombele vya vizara ya Kilimo, Ufugaji na uvuvi na imelenga kutatua changamoto na kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo, Kuongeza pato la Taifa, Kuboresha kipato cha wakulima wadogo na usalama wa chakula na lishe nchini.
Sambamba na hayo pia alisema kuwa wadau wote wa ASDP 2 wanapaswa kusimamia na kutekeleza kwa weledi maeneo makuu manne ya utekelezaji wa Programu hiyo ambayo ni Usimamizi wa Matumizi ya maji na ardhi (Sustainable Water and Land use Management),, Kuongeza tija na faida katika kilimo, mifugo na uvuvi (Enhanced Agricultural productivity and profitability).
Maeneo mengine ya kusimamiwa vyema na wadau ni Biashara na Uongezaji wa thamani kwenye mazao (Commercialization and Value Addition, na Viwezeshi vya sekta, Uratibu, Ufuatiliaji, na Tathmini ya sekta (Sector Enablers, Coordination and Monitoring and Evaluation)