Rais Mhe Dkt. John Pombe Magufuli azindua rasmi program ya ASDP II
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli leo emezindua rasmi programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) hafla ambayo imefanyika
katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, na kuhudhuriwa na makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Dara es salaam Mhe Paul Makonda, Mawaziri wa sekta za kilimo pamoja viongozi wa dini na wadau wote wa sekta ya hiyo.
Akhutubia katika mkutano huo Rais amezitaka sekta za kilimo ,Sekta binafsi na Asasi za kiraia kujumuika pamoja katika kutelekeza mpango huu wa ASDP II ili kuongeza tija katika sekta za Kilimo,Mifugo,Uvuvi na Viwanda.
Hata hivyo Mhe.Rais ameiagiza wizara ya kilimo pamoja na wadau wengine wa kilimo kushughulikia kikamilifu changamoto zote zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa programu hiyo ya awamu ya Kwanza.
Aidha ameongeza kuwa sekta ya kilimo inanafasi kubwa ya kubadilisha hali ya uchumi wa nchi kuliko sekta za madini na gesi hivyo kilimo kiboreshwe ili kiweze kuleta mapinduzi katika sekta nyingine. alisistiza Mhe.Rais
Katika hatua nyingine Mhe. Rais ameitaka Benki ya Kilimo Tanzania (TADB) kusimamia malengo ya kuanzishwa kwake ili iweze kutoa msaada kwa wakulima ikiwemo kuwakopesha badala ya kufanya biashara baina ya benki na kuwakopesha wafanyakazi wake jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.
Awali waziri wa kilimo Mhe. Dkt.Charles Tizeba amesema kwamba
Makadirio ya mahitaji ya rasilimali (Bajeti) kwa ajili ya utekelezaji wa program hiyo ni shilingi Trilioni 13 ambazo zitahitajika kutekeleza mpango huo kwa kipindi cha miaka 5 ya mwanzo.
“tayari kwa mwaka ujao wa fedha wa 2018/19, Serikali unayoiongoza inatarajia kuchangia kiasi cha Shilingi Bilioni 943 kupitia Wizara za Sekta ya Kilimo ambazo ni Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji. Aidha Halmashauri zote za Wilaya kupitia makusanyo yake ya ndani (own sources) zinatarajia kuchangia kiasi cha Shilingi bilioni 36”. Alisisitiza Dkt Tizeba