Ujumbe wa AFDP wakutana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Yonazi
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amekutana na ujumbe kutoka Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) na wataalam wake na kufanya nao mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma kuhusu masuala na maeneo ya ushirikiano katika kutekeleza Program hiyo.
Katika Mazungumzo yao, yaliyofanyika Mei 9, 2023, Katibu Mkuu Dkt.Yonazi alieleza kwa kina jinsi Serikali ilivyo tayari na inavyotoa ushirikiano wa hali ya juu katika kutekeleza Program hiyo huku akifafanua kuwa, kwa wakati serikali inaainisha masuala mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika utekelezaji wake na kuyafanyia kazi kwa kuzingatia taratibu za Serikali.
Nae Mwakilishi Mkazi wa Programu hiyo nchini Bw. Robson Mutendi kwa upande wake alisema wakati wa mazungumzo hayo kuwa, ujumbe huo maalum wa ukaguzi wa maeneo ya mradi, utatembelea katika baadhi ya maeneo ambayo mradi unatekelezeka ikiwa ni njia mojawapo ya kuona na kuainisha maeneo yenye mapungufu, ili kufanyiwa kazi na kufikia malengo na kuomba ushirikiano katika utendaji ili uweze kuleta matokeo tarajiwa chanya.
Baada ya mazungumzo hayo mahususi na Katibu Mkuu, Dkt. Yonaz, ujumbe huo wa AFDP pamoja na wataalam ulipanga kukutana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi pia kumbelea baadhi ya maeneo Programu inapotekelezwa ikiwa ni pamoja na mikoa ya Tabora, Geita, Lindi na Zanzibar.